Image
Image

Serikali imeanza kutumia sheria mpya ya fidia kwa wafanyakazi.


Serikali imeanza kutumia sheria mpya ya fidia kwa wafanyakazi inayolenga kuwaondolea waajiri wajibu wa kumuhudumia mfanyakazi aliyepata ajali kazini kwa kuanzisha mfuko wa fidia kwa wafanyakazi wa serikali na sekta binafsi utakao kuwa na mamlaka ya kisheria ya kulipa fidia ikiwemo gharama za matibabu kwa watumishi watakaoumia kazini.

Akizindua bodi ya wadhamini ya mfuko wa fidia kwa wafanyakazi, waziri wa kazi na ajira Mhe.Gaudencia Kabaka amesema chini ya sheria hiyo waajiri katika sekta binafsi wanapaswa kuwasilisha michango ya asilimia moja ya jumla ya mishahara ya wafanyakazi wote ambapo katika sekta ya Umma mwajiri anapaswa kuwasilisha michango ya asilimia 0.5 katika mfuko huo na kusisitiza sheria hiyo inalenga kuongeza tija na kumuondolea kazi ya kuhudumia wafanyakazi mwajiri.

Awali akielezea kuhusu mfuko huo,mwenyekiti wa bodi ya WCF Bwana.Emmanuel Humba amevitaka vyuo vikuu nchni kuisaidia taasisi hiyo katika kufanya tafiti na kuibua mifumo itakayosaidia kuendesha mfuko huo kisasa katika utoaji wa huduma katika mazingira tofauti ya ajari zinazowakuta watumishi wa umma na sekta binafsi hali itakayosaidia kujenga imani kwa wananchi pamoja na kuongeza uwajibikaji kwa watendaji.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment