Dr.John Pombe Magufuli ambaye ni mgombea urais kupitia chama
cha mapinduzi CCM ameyasema hayo katika wilaya ya ifakara katika mkutano
uliohudhuriwa na makumi kwa mamia ya wananchi ambapo amewataka wale wote wanaohodhi
mashamba makubwa bila ya kuyaendeleza waanze kuyafanyia kazi la sivyo serikali
itayachukuwa yote bila ya kujali wadhifa wa mtu anayeyahodhi ili serikali
iyagawe kwa wananchi wenye mahitaji.
Aidha Dr.Magufuli amewahakikishia wananchi wa maeneo ya ifakara,malinyi
na mahenge mkoani Morogoro ambapo amefanyaka mikutano ya hadhara kwa kutumia
barabara lakini pia kukagu ujenzi wa daraja la mto kilombero na kuwaahidi
watanzania kuw serikali yakem itatilia mkazo suala la kuendelea kuboresha
miundo mbinu ya barabara.
Mjumbe wa kamati kuu na mwenyekiti wa jumuia ya wazazi CCM
Alhaji Abdala Bulembo amewataka watanzania kumchagua Dr. Magufuli kwa kuwa ni
mwadilifu na anachukia rushwa na kwamba ana uwezo wa kupambana na mafisadi
ambapo pia aliyekuwa diwani na mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo
chadema wilaya ya ulanga Bw.Saidi Tira na mratibu wa chadema msingi mkoa wa
Morogoro Evance Tagaya wakitangaza rasmi kukihama chama hicho na kujiunga na
chama cha mapinduzi CCM.
Dr.Magufuli akiwa njiani kutokea wilaya ya mahenge kwenda
ifakara kwa ajili ya kuzungumza na wananchi wa ifakara amekagua ujenzi wa
daraja la mto kilombero na kumtaka mkandarasi kuimaliza kazi hiyo kwa wakati
ili kuwaondolea wananchi adha wanayoipata kwa sasa.

0 comments:
Post a Comment