Watanzania wametakiwa kutoaamini kauli za vyama vya upinzani,kuwa Chama cha Mapinduzi hakijafanya lolote kwani imeboresha huduma za jamii kama elimu, afya, miundombinu, kilimo na huduma kwa makundi maalumu ya vijana, wazee na walemavu kwa asilimia 88.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoani Lindi, AMIRI MKALIPA amesema hayo kwenye uzinduzi wa kampeni ya CCM, Kata ya Mipingo Wilaya ya Lindi Vijijini uliotumika kumnadi mgombea wa udiwani wa kata hiyo.
MKALIPA amesema katika kipindi cha miaka 10 cha utekelezaji wa ilani CCM imejenga shule za sekondari 4,576 sawa na ongezeko la asilimia 162, waalimu waliohitimu Elfu-73 na 407, wakati ujenzi wa barabara za lami imefikia Kilometa Elfu 17.6.
Amewataka Watanzania kukipigia kura Chama cha Mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu ujao, ili kulinda na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana.
Kwenye uzinduzi huo wanachama 10 wa Chama cha Wananchi - CUF akiwemo katibu wa chama hiho wa Kata ya Mipingo wamejitoa chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi.
Home
News
Watanzania wametakiwa kutoaamini kauli za vyama vya upinzani,kuwa Chama cha Mapinduzi hakijafanya lolote.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment