Mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo, ( CHADEMA ),chini ya mwavuli wa vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi ( UKAWA ),Mh.Juma Duni Haji amefanya mikutano ya kampeni za uchaguzi mkuu katika wilaya za Mkinga, Muheza, Pangani na jijini Tanga kwa ajili ya kumuombea kura mgombea urais wa chama hicho Mh. Edward Lowassa na kuhaidi kumaliza tatizo la mgao wa umeme ambalo limekuwa ni kero kubwa kwa wananchi.
Halikadhalika, mgombea mwenza
huyo Mh.Juma Duni haji ameelezea namna serikali ya chama cha mapinduzi chini ya
uongozi wa rais Jakaya Kikwete ilivyoshindwa kutekeleza ahadi ya kulifanya jiji
la Tanga kuwa jiji la viwanda kama alivyohaidi mwaka 2010 wakati akinadi ilani
ya chama hicho iliyomuweka madarakani katika muhula wa pili unaomalizika oktoba
mwaka huu wa 2015.
Katika mikutano hiyo ya
kampeni za uchaguzi mkuu, mgombea mwenza huyo amesema Tanzania ni moja ya nchi
katika bara la Afrika zenye utajiri mkubwa wa raslimali na maliasili ambazo
zikitumika vizuri zinaweza kumaliza kabisa changamoto za umaskini uliotopea,
hivyo amewaomba watanzania kumchagua Mh. Edward Lowassa kuwa rais wa serikali
ya awamu ya tano ili aweze kuboresha mishahara ya wafanyakazi wakiwemo walimu,
kuwasaidia mikopo wakulima, kugharimia matibabu ya bure na kuwasomesha bure
wanafunzi.





0 comments:
Post a Comment