Mkaguzi
wa Dawa wa mamlaka ya chakula na Dawa TFDA kanda ya nyanda za juu kusini Dakta
Sylvester Mwidunda, akiongea wakati wa uteketezaji wa bidhaa hizo zenye madhara
makubwa kwa matumizi ya binadamu,amesema msako huo ni endelevu kwa vile baadhi
ya wafanyabiashara wamekuwa sio waaminifu,na kwamba wamegundua kiwanda kidogo
kinachotengeneza pipi bila ya kufuata taratibu na sheria, na kuweka anuani ya
moshi kwa udanganyifu.
Naye
afisa afya na usafi wa mazingira wa manispaa ya Sumbawanga Bw.sward Temba,
amesema kuwa baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakikamatwa zaidi ya mara moja
wakitenda kosa la kuuza vyakula ambavyo vimepitwa na tarehe zake za matumizi na
pia vipodozi ambavyo vina sumu na vimepigwa marufuku,na kwamba sasa badala ya
kuchangia gharama za uteketezaji wa bidhaa hizo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa
ikiwa ni pamoja na kufikishwa vyombo vya kisheria



0 comments:
Post a Comment