Image
Image

Wakazi wa Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma, wamelalamikia kero mbalimbali za maji.

Wakazi wa Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma, wamelalamikia kero mbalimbali za maji na barabara inayounganisha mkoa huo na mikoa jirani.
Wamesema  kwa zaidi ya miaka hamsini ya uhuru barabara hiyo haijajengwa na hivyo kusababisha kuongezeka kwa ujambazi na utekaji magari  pamoja na kutokukua kwa uchumi kutokana na miundombinu duni.
Wakizungumza katika mahojiano na Radio One Stereo  wamesema  licha ya barabara ya Kigoma-Kasulu kupitia Kakonko hadi Nyakanazi yenye Kilomita 300  kuwa na umuhimu mkubwa kwa  uchumi wa Mkoa wa Kigoma na taifa pamoja na ulinzi na usalama  kutokana na kuwa mpakani.
Wakazi hao wamewataka viongozi watakaochaguliwa katika uchaguzi mkuu ujao kuipa kipaumbele barabara hiyo ili kurahisisha mawasiliano kati ya Mkoa wa Kigoma na mikoa jirani.
Akizunguzia barabara hiyo katika kampeni za Chama cha Mapinduzi katika Jimbo la Buyungu Kakonko, Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -  Uwekezaji na Uwezeshaji na mgombea ubunge wa CCM katika jimbo hilo, CHRISTOPHER CHIZA amesema tayari ujenzi wa barabara hiyo umeanza na kwamba mgombea Urais  wa CCM Dakta JOHN POMBE MAGUFULI ataikamilisha barabara hiyo baada ya kushika madaraka.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment