Image
Image

Mawakala wa ununuzi wa Pamba watuhumiwa kuua bei ya soko la Pamba ya Tanzania .


Mawakala na wanunuzi wa Pamba mkoani Shinyanga wametuhumiwa kuua soko la zao hilo nchini kwa kuharibu ubora wake kwa kuchanganya mchanga,mawe na maji baada ya kununua kutoka kwa wakulima ili kuongeza uzito hali ambayo imesababisha bei ya pamba kushuka na kutishia kufungwa kwa wiwanda vya kuchambua pamba na kusababisha ukosefu wa ajira kwa asilimia kubwa ya wakazi wa mkoa huo.
Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa viwanda vinavyochambua Pamba mkaguzi mkuu wa Pamba wilayani Kahama Bw.Emmanuel Kileo amesema pamoja na bodi ya Pamba nchini kutoa elimu juu ya usafi na ubora wa zao hilo kwa wakulima na wanunuzi lakini bado wahusika wanafanya makusudi ili mkujipatia maslahi yao binafsi na kusababisha soko la pamba ya tanzania kuporomoka.
Mmoja wa mawakala anayetuhumiwa kuweka mawe yenye uzito wa tani tatu katika mzigo wa pamba wenye uzito wa tani kumi na mbili Bw.Marwa Jackson kutoka katika kampuni ya nida amedai tatizo hilo haliko upande wake bali ni mipango ya wakulima na wapakiaji kutoka katika maeneo ya ununuzi kutaka kumharibia kazi yake.
Nao baadhi ya wakulima wa pamba waliokuja kushuhudia rundo la mawe na mchanga uliokua umechanganywa na pamba wamesema wanashangaa kusingiziwa kuchafua pamba huku meneja mkuu wa kiwanda cha kuchambua pamba cha nida Bw.Mohamed Ackbar akiitaka serikali kuunda mfumo mpya juu ya ununuzi wa pamba kwakua hali hiyo inatishia kufilisi wawekezaji na kupoteza ajira ya vijana wengi waliokua wameajiriwa katika viwanda vya kuchambua pamba.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment