MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli,
amesema kama atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
katika uchaguzi mkuu ujao, Serikali yake haitakuwa na maadhimisho ya
Wiki ya Maji.
Dk. Magufuli, aliyasema hayo jana alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni wa kuomba kura za kuchaguliwa mjini hapa.
Wiki ya Maji kitaifa huadhimishiwa Machi 16 hadi 22 kila mwaka,
ambapo viongozi mbalimbali wa kitaifa huzindua miradi ya maji vijijini
na mijini na kuweka mawe ya msingi.
Kwa mwaka huu, wiki hiyo iliadhimishwa kitaifa mkoani Mara.
Dk. Magufuli alisema inashangaza kuona watu wanafanya maadhimisho
hayo, huku mamilioni ya fedha yakitumika, na wananchi wakiendelea kukosa
maji mijini na vijijini.
Alisema hakuna haja ya kuwa na maadhimisho hayo, kwa sababu yanaonekana hayana faida kwa wananchi.
“Mimi nimeomba urais sio kwa majaribio, ninajua matatizo ya Watanzania,
ndiyo maana nasema na ninajua hapa hakuna maji, kule juu wanatafuta
fedha kwa maadhimisho ya Wiki ya Maji wakati watu hawana maji.
“Kama mtanichagua, Serikali yangu ya awamu ya tano itafuta maadhimisho haya, fedha nyingi zinatumika.
“Kuchimba kisima kimoja hakizidi Sh milioni 25 na Waziri wa Maji
nitakayemteua atakuwa na kazi ya kuleta maji na si kila siku tuko kwenye
mchakato.
“Akiwa na lugha hii itabidi akae pembeni ili akajichakatue mwenyewe,
sikubali hata kidogo. Kikubwa nawaomba mniamini na mnichague ili nianze
kazi hii kwa kasi ya kuwatumikia,” alisema Magufuli.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment