Image
Image

Watanzania watakiwa kutambua umuhimu wa mitandao ya kijamii.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, LUDOVICK MWANANZILA amewataka wananchi wa mkoa huo na Tanzania kwa ujumla kutambua umuhimu wa sheria ya mtandao iliyotiwa  saini na serikali, kuwa imelenga kuwanusuru na unyanyasaji wa kijinsia.
Amesema awali hapakuwepo na jinsi ya kumlinda mtendewa ili apate haki yake, ikiwa ni pamoja na kudhibiti wizi wa fedha katika mitandao, pamoja na kugushi nyaraka za serikali.
Mkuu huyo wa mkoa wa tabora  ametoa rai hiyo,  wakati akifungua warsha elekezi kwa mahakimu,  mawakili wa serikali, Waendesha Mashitaka wa Serikali, na  maafisa wapelelezi wa wilaya,  kutoka katika wilaya zote za mikoa ya Kigoma, Katavi, Shinyanga, na Tabora.
Warsha hiyo imeandaliwa na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Tekinolojia, inayolenga kuwajengea uwezo  wa matumizi sahihi ya usalama wa mitandao.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment