Image
Image

Wizara ya Maliasili na Utalii na WWF wanaadhimisha siku ya tembo kitaifa.

Wizara ya Maliasili na Utalii ikishirikiana na Shirika la Uhifadhi Duniani -WWF Ofisi ya Tanzania  kwa pamoja leo wanaadhimisha siku ya tembo kitaifa mwaka huu.
Katika maadhimisho hayo wadau watapata nafasi ya kujadili namna ya kumuokoa mnyama Tembo kupitia vyombo vya habari hapa nchini.
Malengo ya kuadhimisha siku ya Tembo kitaifa ni kujenga uelewa na kuibua hamasa ya wananchi kuhusu uhifadhi wa tembo, kujadili kwa kina madhara ya ujangili wa Tembo katika nyanja za jamii, kiikolojia, kiutamaduni na sekta ya utalii kwa jumla na kutoa mapendekezo na hatua za kuchukua kuzuia ujangili wa Tembo.
Maadhimisho haya yanatokana na mkutano wa 15 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa kuzuia biashara ya Wanyamapori na viumbe walioko hatarini kutoweka.
Kauli Mbiu ni 'WAKATI WA KUHIFADHI TEMBO WALIOSALIA NI SASA.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment