Vita hivyo viliwauawa zaidi ya milioni 15 ya raia wa China.
Lakini siku hizi, Beijing imekua ikijisifu kama taifa lililokua zaidi katika
sekta mbalimbali. Hayo aliyazungumza Rais Xi Jinping katika hotuba yake.
Kama watawala, ambao walipata uhalali wao kutoka mbinguni,
Rais akiwa pia Mkuu wa jeshi la Jamhuri ya Watu wa China ameweza kusalimia
askari wake, huku akisimama katika gari lake leusi, aina ya a limousine, katika
jua kali kwenye barabara iliyopewa jina la Amani ya Mbinguni (Tianamnen).
Kutoka juu ya mlango wa kusini kwa mji, ambapo Mao
alitangaza kuzaliwa kwa taifa la watu wa China tarehe 1 Oktoba mwaka 1949, Xi
Jinping amewahutubia askari 12,000 ambao walikua wakimuangalia na kumfuata kwa
makini anavyozungumza. "Mumefanya kazi kubwa ", amesema Xi. "Kwa
kuwahudumia wananchi! ", askari walijibiu.
Askari wa China walivaa sare mpya za jeshi, na kuongeza
bidhaa mbalimbali za China, amesema mwandishi wetu mjini Beijing, Heike Schmidt.
Zaidi ya 80% vifaru, makombora, ndege za kivita za kisasa, magari 500 kwa
jumla, pia yalionekana katika umma kwa mara ya kwanza. Kati vifaa hivyo, maelfu
ya makombora mapya ya jeshi la China, DF-21D. Silaha hizi, ambazo zinaweza bado
kupima takriban upeo, zinaongeza kwa miaka kadhaa katika mjadala katika maeneo
ya kijeshi juu ya uwezo wao wa kubadilisha uwezo wa nguvu katika Bahari ya
Pasifiki.

0 comments:
Post a Comment