MAMA mtoto wa Chris Brown, Nia Guzman, ameweka wazi kwamba hakuwahi
kuwa na uhusiano wa kimapenzi na raia wa Brazil, King Ba ambaye alidai
kuwa mtoto aliyezaa na mwanamuziki, Chriss Brown ni wake.
Awali msanii huyo alichafua hali ya hewa baada ya kutangaza kuwa
ndiye baba wa mtoto huyo, Royalty ambaye ni mtoto wa Chris Brown.
“Sikuwa na uhusiano wowote na King Ba zaidi ya urafiki tu, habari
zote ni uhongo, ukweli ni kwamba Chris ni baba sahihi wa mtoto huyo
japokuwa nina wasiwasi na usalama wa mwanangu kutokana na tabia za
msanii huyo,” alieleza Nia.
Hata hivyo, Chris ameonekana kutulia tangu alipofanikiwa kumpata
mtoto huyo na kudai kuwa ameamua kubadilika ili aonekane baba mwema.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment