Shirika la Utafiti na Tiba Barani Afrika - AMREF kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ,linaendelea kuwajengea uwezo wa kitaaluma wauguzi kwa njia ya elimu mafasa kupitia vyuo 26 vya hapa nchini ambavyo tayari vimeingizwa katika mfumo wa elimu ya uuguzi kwa njia ya elimu masafa.
Hayo yalielezwa na Kaimu Mkurugenzi wa shirika hilo,Dakta PIUS CHAYA wakati wa mafunzo ya wakuu wa vyuo hivyo vya uuguzi yaliyolenga kuwaongezea uwezo wa kufikisha elimu hiyo ya masafa kwa wauguzi wenye elimu ya cheti na kufikia kiwango cha shahada na stashahada .
Dakta CHAYA amesema mfumo huo wa utoaji elimu ya uuguzi kwa njia ya masafa ulianza mwaka 2013 na kuvihusisha vyuo 10 na kwa sasa tayari umeshafikishwa katika vyuo 26 vya uuguzi , ambavyo ni vya mashirika ya dini na serikali.
Na y e D akta HERILINDA TEMBA akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro amesema idadi ya wauguzi hapa nchini , hasa maeneo ya vijijini ni ndogo hali inayosababisha muuguzi mmoja kuhudumia wagonjwa 5000 kwa mwaka .
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment