Image
Image

Bi.Clinton awatupia lawama wapinzani wa chama cha Republican.

Anayedhaniwa kuwa mstari wa mbele katika uteuzi wa Urais katika chama cha Democratic, Hillary Clinton, amewalaumu wapinzani wake wa chama cha Republican kwa kutumia vifo vya wanadiplomasia nchini Libya kujinufaisha kisiasa.
Bi Clinton amekuwa akitoa ushahidi mbele ya Kamati ya Bunge la Congress inayochunguza shambulizi katika ubalozi wa Marekani nchini Libya, katika mji wa Benghazi mwaka 2012 alipokuwa Waziri wa Mashauri ya Kigeni.
Alisema alijiwajibisha kwa kukubali kosa hilo ambapo watu wanne walifariki, kukiwemo balozi Christopher Stevens.
Mwanachama mkongwe wa kamati huyo kutoka chama cha Democratic, Elijah Cummings, alisema kuwa uchunguzi huo unaoongozwa na chama cha Republican ni matumizi mabaya ya sheria yenye lengo la kumvurugia Bi Clinton kampeni yake ya kutaka kuwa Rais wa Marekani.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment