Dlamini-Zuma, kiongozi wa Umoja wa Afrika amefahamisha
kumteua Francisco Caetano Jose Madeira kutoka Msumbiji kuwa muakilishi
maalumu wa AMISOM nchini Somalia.
Francisco Caetano Jose Madeira anachukuwa wadhifa wa balozi Maman Sidikou ambae alikuwa
akiongoza AMISOM tangu mwaka 2010.
Madeira atashirikiana na serikali ya Somalia, UN, Umoja wa
Ulaya, Marekani na Uingereza katika harakati za kusaka amani nchini humo.
Madeira aliwahi kuongoza idara mbali mbali Umoja Wa Afrika
moja wapo katika kitengo cha kupambana na ugaidi ambapo alipambana na waasi wa
Uganda kati ya mwaka 2011 na 2014.
Tangu mwaka 2006 jeshi la Somalia linashirikiana na vikosi
vya Umoja wa Afrika dhidi ya kundi la wanamgambo wa al Shabaab wanaodai kutaka
kuweka sheria za kiislamu.
0 comments:
Post a Comment