Wasiwasi umezuka katika mji wa Calabar, kusini mwa Nigeria
baada ya mtu mmoja kufariki baada ya kuonyesha dalili zinazokaribia za ugonjwa
wa Ebola.
Shirika la usimamizi wa mambo ya dharura nchini humo
linasema kuwa watu kumi wamewekwa karantini baada ya kugusana na mtu
aliyeonekana kuwa na dalili za ugonjwa huo.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema mtu huyo alifariki
punde baada ya kufikishwa hospitalini.
Sampuli za damu kwa sasa zinafanyiwa uchunguzi.
Shirika la afya duniani WHO lilitoa taarifa yake siku ya
Jumatano kuwa nchi tatu zilizokuwa zimeathiriwa kwa kiasi kikubwa na ugonjwa
huo ambazo ni Guinea, Sierra Leone na Liberia, zimefanikiwa kukaa wiki moja
bila kuwa na tukio lolote la ugonjwa wa Ebola kwa mara ya kwanza kabisa tangu
kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa huo mwezi Machi mwaka 2014.
Zaidi ya watu 11,000 walifariki dunia kwa ugonjwa huo.
0 comments:
Post a Comment