Umoja wa Ulaya (EU) umetangaza mpango wake wa kutuma
wajumbe zaidi 80 nchini Burkina Faso kwa ajili ya kusimamia na kufuatilia uchaguzi.
EU ilitoa maelezo siku ya Alhamisi na kusema kwamba wajumbe
24 wataelekea Burkina Faso wiki tatu kabla ya uchaguzi huku wengine zaidi ya 48
wakitarajiwa kuwasili nchini humo siku yauchaguzi.
Msimamizi mkuu wa wajumbe hao wa EU Cecile Kashetu Kyenge
tayari amewasili mjini Ouagadougou ili kuanzisha shughuli za maandilizi ya uchaguzi.
Wakati huo huo, EU pia imetoa msaada wa vifaa vya uchaguzi
kwa tume ya kitaifa ya kujitegemea ya uchaguzi nchini
Burkina Faso.
Uchaguzi uliotarajiwa kufanyika tarehe 11 Oktoba nchini
Burkina Faso, ulilazimika kuahirishwa hadi tarehe za mbeleni kutokana na
jaribio la mapinduzi lililotekelezwa tarehe 16 Septemba.
0 comments:
Post a Comment