Shrikila la Misaada ya Vyakula Duniani WFP, limetangaza
mpango wake wa kutoa misaada ya vyakula kwa wananchi 850,000 wanaokumbwa na baa la njaa nchini Zimbabwe.
Uhaba wa mvua,ukame wa maji na hali mbaya ya hewa
iliokuwepo katika misimu ya miaka 2014-2015, imeathiri vibaya sekta ya kilimo
nchini Zimbabwe na kupunguza mavuno ya vyakula.
Kiwango cha mazao ya mahindi kimepungua kwa asilimia 40
katika mwaka wa 2015 nchini Zimbabwe na kuilazimu serikali kununua tani 700,000
za mahindi kutoka nje.
Kulingana na takwimu zilizotolewa na kamati ya utafiti,
kuna takriban wananchi milioni 1.5 wanaoishi katika vijiji vya Zimbabwe
wanaokabiliwa na baa la njaa.
WFP imetangaza kwamba itatoa misaada ya vyakula na
kuchangia fedha dola milioni 18.5 kwa ajili ya kukabiliana na baa la njaa nchini Zimbabwe.
0 comments:
Post a Comment