MKOA wa Arusha umefunika! Hii ndiyo kauli unayoweza kuitoa kutokana
na umati mkubwa wa wananchi uliojitokeza kumsikiliza mgombea urais wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.John Magufulu, huku mgombea huyo
akiwaeleza wazi wananchi hao kuwa, wamefunika na hakunaga kama mkoa huo.
Ujio wa Dk.Magufuli mkoani Arusha umeonesha namna ambavyo maelfu ya
wananchi wameamua na wako tayari kumpa ridhaa ya kuwatumikia katika
Serikali ya awamu ya tan, huku akitumia nafasi hiyo kuwahakikishia
wananchi hao kwamba, yeye ni kazi tu na hatawaangusha.
Dk.Magufuli akiwa mkoani hapa jana, alizungumzia mambo ya msingi
atakayofanya kwenye Serikali yake ya awamu ya tano, hivyo aliomba
wananchi kumchagua kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka
huu, na kutumia nafasi hiyo kutoa salamu kwa waliokuwa na viwanda,
wakashindwa kuviendeleza.
Akizungumza mbele ya wananchi hao, Dk.Magufuli alisema ameamua kuomba
ridhaa ya kuwania urais kwa kutambua anaiweza nafasi hiyo na ndiyo
maana wale mafisadi na majizi baada ya kuona jina lake limepitishwa na
CCM, walianza kukimbia, na wanaotesa wananchi hivi sasa kwa kukata umeme
wajiandae kwani, atawashughulikia.
Dk.Magufuli alisema anatambua hiki ni kipindi cha kampeni na mawaziri
ambao wanahusika na nishati ya umeme wapo kwenye majimbo wakiomba
kampeni, lakini wahakikishe umeme haukatiki na iwapo utaendelea na yeye
akachaguliwa kuwa rais, mawaziri hao wajiandae kuondoka na kabla ya
umeme kukatika, basi atawakata wao.
Alisema anatambua changamoto za maisha ambazo wanakumbana nazo na
yeye kwenye Serikali atakayound, atahakikisha anatafuta ufumbuzi wake na
hilo litafanikiwa kwa kufanya kazi akishirikiana na mawaziri na
watendaji wengine atakaowateua.
Kwa Mkoa wa Arusha, Dk.Magufuli alisema anatambua kulikuwa na Kiwanda
cha General Tyre na Kiltex ambavyo kwa sasa vimekufa, lakini aliahidi
akipata urais, atahakikisha vinafufuliwa na waliopewa kama watashindwa
kuviendelez, wajiandae kuvirudisha na kwenye hilo hatashindwa.
“Serikali ya awamu ya tano chini ya utawala wangu iwapo nitapata
ridhaa, nitahakikisha viwanda hivi vya Arusha vinafanya kazi. Lengo ni
kuboresha maisha ya wananchi wetu kwani, Arusha kuna kila kitu hivyo,
haiwezekani waendelee kuteseka,” alisema Dk.Magufuli.
Aliongeza, yeye hajui siasa, bali kwake ni kazi tu na kuwaomba
wananchi hao wamchague awe rais na hawatajuta kwa kumpa nafasi hiyo na
kuongeza kuwa, anajua kujitoa kwa watu wake na ndiyo maana akiwa Waziri
wa Ujenzi ilifika mahali akalala nje kwa ajili ya kusimamia ujenzi wa
madaraja.
Alisisitiza Serikali ya Magufuli kazi yake kubwa itakuwa ni
kutengeneza viwanda vya kutosha na anatambua kuwa, hilo kwake
linawezekana na tayari Ilani ya uchaguzi mkuu ya chama hicho imejipanga
vizuri kuwatumikia wananchi na kuongeza, mabadiliko ya kweli yatatokana
na Magufuli.
Alitumia nafasi hiyo kuwaeleza wananchi kuwa, huu ni wakati wa
Magufuli kwa mabadiliko(Magufuli for Change), ambapo aliitaja kwa kifupi
M4C.
Wakati mkutano huo wa kuomba kura, Dk.Magufuli aliwapokea wanachama
wapya kutoka vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),
wakiwamo waliokuwa waratibu wa maandamano ya Chadema mkoani Arusha,
ambao walisema hawawezi kubaki Chadema wakati waliokuwa wakimtuhumu kwa
ufisadi amekimbilia upande huo.
Akiwa Monduli
Akiwa Monduli
Akiwa wilayani Monduli, Dk.Magufuli alisema kuwa, nafasi ya kuwa rais
inanukia kwa kasi, hali inayomfanya kuamini kuwa, atakuwa rais wa awamu
ya tano kwa maana hakuna kipingamizi.
Aliongeza kuwa, ili kusukuma maendeleo katika mji huo, atahakikisha
mabwawa 13 yaliyojengwa na marehemu Waziri Mkuu wa zamani, Hayati Edward
Sokoin, ambayo baadhi yake yamebomoka, yanajengwa tena.
“Huwezi kutamka Monduli bila kutaja jina la Sokoine, kwa maana
alifanya kazi kubwa ambayo haitasahaulika Tanzania na Dunia, ninataka
nifanye kazi kama yeye,” alisema.
Aliwaomba wananchi hao kuipigia kura CCM, kwa maana ndicho chama cha
ushindi na kuwaomba wasipoteze kura kwa vyama vya upinzani ambavyo si
washindi katika uchaguzi huo.
Akiwa Jimbo la Monduli , Dk.Magufuli aliwahakikishia wananchi hao
namna ambavyo amejipanga kuwatumikia kwa dhati, ambapo wakati akihutubia
mkutano wake uliohudhuriwa na raia wa kigeni waliokuwa wamevaa kofia za
CCM, walikuwa wakishangilia.
Dk.Magufuli alitumia nafasi hiyo kumnadi na kumwombea kura mgombea wa
jimbo hilo, Namelok Sokoine, ambaye ni mtoto wa hayati Sokoine,
aliyefariki dunia kwa ajali ya gari mwaka 1984, wakati akitokea mkoani
Dodoma bungeni akielekea Dar es Salaam.
Dk. Magufuli aliwaomba wananchi hao kumchagua Namelok kwa ajili ya
kuendeleza taswira ya Sokoine ambaye enzi za uhai wake wa uongozi,
alikataa ufisadi na rushwa, jambo ambalo lilimjengea heshima kubwa ndani
na nje ya nchi.
Wakati huo huo, Dk. Magufuli alimtaka Namelok pindi atakapochaguliwa
kuwa mbunge wa jimbo hilo, kuhakikisha anatatua kero za wananchi na
kuwaletea maendeleo yanayohitajika.
Moja ya kero ambayo Dk.Magufuli alimtaka Namelok kuishughulikia, ni
kuhakikisha Meneja wa Shirika la Umeme (Tanesco), Mkoa wa Arusha
kupelekea ofisi wilayani Monduli ili kurahisisha shughuli za kiutendaji,
ikiwemo upatikanaji wa luku.
Akiwa nyumbani kwa Waziri Sokoine, Dk. Magufuli alikutana na mjane wa
marehemu Sokoine na kukagua nyumba inayojengwa kwa ajili ya makazi
mapya ya wanafamilia hao.
Kinana afunguka
Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika mkutano
huo, alisema wale wachache wenye mashaka wanapoteza muda wao.
Kinana alifafanua kuwa, tangu mwanzo wa kampeni, CCM inaonesha kupata
ushindi mkubwa na Magufuli ndiye atakayekuwa rais wa Tanzania kutokana
na mwitikio wa wananchi wanavyojitokeza.
Ahadi ambazo Rais Jakaya Kikwete hajazikamilisha, Dk. Magufuli
atazifanyia kazi za kutosha kwa maana ni mchapakazi hodari na mwaminifu.
Aliwataka wananchi kuhakikisha wanafanya uamuzi sahihi katika
kuchagua viongozi wakati wa uchaguzi mkuu Oktoba 25, mwaka huu, na
kuwaomba wasipige kura kwa ushabiki, badala yake wachague kiongozi kwa
maslahi ya nchi yetu, hasa katika kuleta maendeleo na chagua sahihi ni
Dk.Magufuli.
Kinana alisema anatambua katika kipindi cha miaka 50, kuna mambo
mengi yamefanyika nchini, lakini kuna changamoto zilizopo ambazo mwenye
uwezo wa kuzitatua ni Dk.Magufuli na anamwamini anaweza kazi hiyo.
Alisema Serikali ya awamu ya tano inatakiwa kuendelea pale ambapo
Rais Kikwete ameishia na kuongeza, mwenye uwezo huo ni Dk.Magufuli
ambaye atapambana na kila aina ya changamoto, huku akielezea adha ya
umeme ambayo inawakumba wananchi wa Mkoa wa Arusha.
“Kuna tabia ya halmashauri kunyanyasa wafanyabishara kwa kuwatoa
ushuru mara kwa mara, hivyo chini ya Magufuli ataondoa ushuru ambao ni
kero kubwa kwa wananchi,”alisema Kinana.
Ole Sendeka
Ole Sendeka aliwaonya Watanzania kutochagua vyama kwa misingi ya
udini ili visiwagawe kama baadhi ya mataifa yalivyogawanyika kutokana na
udini.
Alisema kuwa, Watanzania wanatakiwa kuchagua rais anayechukia rushwa
na Dk. Magufuli ndiye mpambanaji wa masuala hayo hivyo, wananchi ni vema
wakamchagua kwa kura nyingi.
Sendeka aliongeza kuwa, hata maandamano yaliyokuwa yakifanyika Arusha
yalikuwa ni ‘dili’ alilodai kupangwa na Mbunge wa Arusha Mjini,
Godbless Lema, na kuwataka wananchi hao kumkataa kama ukoma.
Alidai kuwa, mbunge huyo alikuwa akiyapanga maandamano kwa
kushirikiana na wafanyabiashara wa mahoteli nje ya mkoa huo ili
kujipatia fedha.
“Yanapopangwa maandamano na mabomu yanapopigwa, baadhi ya watu
hukimbia na kwenda kulala hotelini na kufanya biashara hiyo, biashara
ambayo Philemon Ndesambulo, Freeman Mbowa waliyakataa na katika majimbo
yao na kutaka vijana wao wafanyekazi,” alisema.
0 comments:
Post a Comment