Image
Image

FAINALI za nne za shindano la Bongo Stars Search zinafanyika leo.

FAINALI za nne za shindano la Bongo Stars Search zinafanyika leo katika ukumbi wa King Solomon huku mshindi wa kwanza anatarajiwa kuondoka na kitita cha Sh milioni 50.
Kila mshiriki anaonekana kujiamini zaidi huku kila mmoja akitamba kuibuka na ushindi wa shindano hilo ambapo mshindi mbali na kuondoka na kitita hicho, atalamba mkataba wa kusimamiwa kazi zake za sanaa na hivyo kufanya kuwa na thamani ya milioni 60.
Kila mmoja anaonesha kuwa na imani na ushindi huku wakionesha uwezo wao wa kuimba pamoja na kucheza.
Washiriki wa mwaka huu ni Frida Amani, Kayumba Juma, Angel Kato, Nassib Fonabo, Jaqline Kakenzi na Kelvin Gerson. Frida Amani anasifika zaidi kwa uwezo wake wa kughani, ambapo amekuwa akiimba rap tangu alipoteuliwa kutokea mkoani Arusha.
Angel Kato yeye anaweza kuimba na kurap pia ni mwanadada mwenye kipaji cha hali ya juu. Kelvin Gerson kama afanyavyo Kayumba Juma na Jackline Kakenzi wao wanaimba na kucheza
huku Nassib Fonabo yeye akihusisha zaidi upigaji wa gita.
Kiingilio cha shindano hilo ni Sh 25, 000, 50,OOO na 100,000. Kutakuwa na burudani kutoka kwa msanii Run Town wa Nigeria ambaye ameshawasili nchini na pia msanii Christian Bella,
Yamoto Band, Peter Msechu, Kala Jeremiah, Navy Kenzo na Ben Pol.
Wadhamini wa shindano hilo kwa mwaka huu ni pamoja na Huawei, Salama Condom, Coca- Cola, Kiwi, Fast Jet, Jubilee Insurance, Radio Clouds na Regency Hotel.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment