Mshukiwa mmoja anayedaiwa kulifadhili kundi la Boko Haram,
ameripotiwa kutiwa mbaroni na jeshi katika mkoa wa Borno ulioko kaskazini
mashariki mwa Nigeria.
Mshukiwa huyo anaarifiwa kupatikana na kiasi cha fedha dola
5,024 pamoja vifaa vingine wakati alipokamatwa na jeshi.
Uchunguzi uliofanyika unaonesha kwamba mshukiwa huyo
amekuwa akiwasambazia wanamgambo wa Boko Haram fedha na vifaa mbalimbali kama
vile dawa za kupoteza usingizi.
Maelezo zaidi yanaarifu kwamba wanamgambo wa Boko Haram pia wamekuwa
wakisambaziwa kokwa za karanga wanazotumia ili kuwakosesha usingizi na
kuwasaidia kuendesha shughuli zao usiku.
Mshukiwa huyo pia anadaiwa kukusanya misaada ya kifedha kutoka kwa wafadhili
wengine wanaounga mkono kundi la Boko Haram na kuwafikishia katika kambi zao.
0 comments:
Post a Comment