Image
Image

Jeshi la Polisi Mbeya linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kutuma picha za udhalilishaji wa viongozi wa kisiasa kwenye mitandao ya kijamii.


Zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya watanzania kupiga kura kuwachagua madiwani, wabunge na rais, Jeshi la polisi mkoani mbeya linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kutengeneza na kutuma kwenye mitandao ya kijamii picha za udhalilishaji wa kiongozi mmoja wa chama cha siasa nchini, huku pia picha hizo zikitoa kashfa na uchochezi kwa wagombea wa vyama vingine vya siasa, jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya mitandao.

Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya,Ahamed Msangi amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni ramadhan juma suma maarufu kwa jina la rama bajaj, mkazi wa forest jijini mbeya ambaye anadaiwa kutengeneza picha za udhalilishaji wa kiongozi mmoja wa chama cha siasa nchini na kuzituma kwenye mitandao ya whatsapp, facebook, istagram na twitter, huku picha hizo zikitoa kashfa kwa wagombea wa vyama vingine, jambo ambalo kamanda msangi amedai kuwa ni kinyume cha sheria ya makosa ya mitandao namba 14 ya mwaka 2015.

Katika hatua nyingine kamanda msangi amewataka wananchi wenye sifa ya kupiga kura wasiogope kwenda vituoni kupiga kura kwa kuwa jeshi hilo limejipanga kuhakikisha kuwa wanakuwa salama wakati wote wa zoezi la pupiga kura.

Uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na rais unatarajiwa kufanyika keshokutwa ambapo wananchi wameaswa kurudi majumbani mwao baada ya kupiga kura ili kuepuka kukinzana na sheria inayokataza kufanya mikusanyiko isiyo na kibali.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment