Rais JAKAYA MRISHO KIKWETE amewaasa wabunge wa Bunge la Msumbiji kuwa na mazungumzo ili kuondoa tofauti zao.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasilino ya Rais Ikulu, kwa vyombo vya habari, Rais KIKWETE ametoa ushauri huo alipozungumza na Spika wa Bunge la Msumbiji Bibi VERONICA MACAMO ofisini kwake Mjini Maputo.
Amewaasa wabunge wasikubali nchi yao kuingia katika vita na badala yake wakae na kuweka makubaliano ambayo yatakubalika kwa vyama vyote na hatimaye kuwaepushia wananchi wa Msumbiji kuingia kwenye vita kwa mara nyingine.
Kikao cha Rais KIKWETE na Spika MACAO ambaye anatoka Chama Tawala cha Ukombozi wa Msumbiji, The Mozambique Liberation Front - FRELIMO- pia kimehudhuriwa na wabunge wa vyama vya Mozambique Democratic Movement na Mozambican National Resistance -RENAMO- ambavyo vinaunda Bunge la Msumbiji.
Rais KIKWETE yupo nchini Msumbiji kwa ziara rasmi ya siku mbili kuanzia jana kufuatia mwaliko kutoka kwa Rais FILIPE JACINTO NYUSI wa Msumbiji.
Jana usiku, Rais NYUSI alimuandalia Rais KIKWETE na Ujumbe wake dhifa kwa Heshima ya Rais KIKWETE ambaye pia katika mazungumzo yao, Rais Kikwete ameaga na kueleza kuwa Tanzania inatarajia kupata kiongozi mwingine baada ya uchaguzi wa tarehe 25 mwezi huu.
0 comments:
Post a Comment