Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu (ACHPR), Jaji
Augustino Ramadhani amewataka wabunge barani Afrika kuzishinikiza nchi zao
kuridhia itifaki ya haki za binadamu iliyokubaliwa miaka 18 iliyopita.
Akihutubia Mkutano wa kwanza wa Kawada wa Kikao cha Nne cha
Umoja wa Mabunge Barani Afrika, Midrand, Afrika Kusini juzi, Jaji Ramadhani
ambaye pia ni Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania alisema kwamba nchi 25 bado
haziridhia itifaki hiyo.
Alisema pia kwamba nchi 47 kati 54 wananchama wa Umoja wa
Afrika (AU) hawakubali azimio linaloruhusu watu binafsi na mashirika yasiyo ya
kiseriakli (NGOs) kufungua kesi moja kwa moja mbele ya Mahakama hiyo yenye
makao yake makuu mjini Arusha, Tanzania.
''Ninawasihi waheshimiwa kuziomba serikali za nchi zenu
kuridhia Itifaki hiyo na kulikubali azimio linaloruhusu watu binafsi na
mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kuja moja kwa moja mbele ya Mahakama ya Juu
ya Haki za Binadamu barani,'' Jaji Ramadhani alisisitiza.
Tangu Itifaki hiyo ipitishwe mwaka 1988, ni nchi 29 tu ndizo
zilizoridhia hadi sasa.
Nchi hizo ni pamoja na Algeria, Benin, Burkina Faso,
Burundi, Cameroon, Ivory Coast, Comoro, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)
, Gabon, Gambia, Ghana, Kenya, Libya, Lesotho, Malawi, Mali, Mauritania,
Msumbiji ,Nigeria, Niger, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kiarabu ya Sahrawi,
Senegal, Afrika Kusini,Tanzania, Togo and Tunisia.
Hadi sasa ni nchi saba tu ambazo zimekubali azimio la
kuruhusu watu binafsi na NGOs kufungua kesi mbele ya ACHPR. Nchi hizo ni pamoja
na Burkina Faso, Ivory Coast, Ghana, Malawi, Mali, Rwanda na Tanzania.
Tangu kuanzishwa kwake mahakama hiyo imeshashughulikia kesi
40.
0 comments:
Post a Comment