Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam imeahirisha kesi ya kikatiba
kuhusu kutoa tafsiri ya umbali wanaotakiwa kusimama wapiga kura baada ya
kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu ili kutoa muda kwa upande wa
serikali kuandaa majibu.
Awali
katika Kesi hiyo inayoongozwa na jaji Sakieti Kihiyo, Aloysious
Mujulizi na Lugano Mwandambo walimtaka wakili wa mpigakura Amy Kibatala,
aliyefungua kesi hiyo kubadilisha hati ya mashitaka kutoka kwa
mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na kuielekeza kwa mkurugenzi wa tume ya
uchaguzi ambaye ndiye mwangalizi wa masuala yote ya uchaguzi.
Kwa upande wao wadaiwa katika kesi hiyo upande wa serikali ikiongozwa
na wakili Obadia Kameya umeiomba mahakama kuipa muda mpaka saa nane
mchana hii jana ili waweze kuwasilisha majibu ya maombi ya kesi hiyo.
Katika kesi hiyo namba 37 ya mwaka 2015 inayosimamiwa na wakili Peter
Kibatala inaiomba mahakama kutoa tafsiri sahihi ya kifungu cha 104 (1)
cha sheria ya taifa ya uchaguzi kuhusu umbali ambao mpiga kura
anastahili kukaa kutoka kituo cha kupigia kura.
Jaji Sakieti Kihiyo ambaye ni mwenyekiti wa kesi hiyo ameahirisha kesi hiyo mpaka leo saa tatu itakaposikilizwa tena.
0 comments:
Post a Comment