Watu kumi na saba wamefariki dunia na wengine 785 walilazwa katika vituo vinne vya afya kutokana na ugonjwa wa Kipindupindu katika halmashauri ya wilaya ya Singida kati mwezi uliopita na mwezi huu.
Kaimu Mganga wa Mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Singida, Dakta PAUL MAIGA amesema hayo, wakati akipokea vibuyu chirizi elfu nne mia sita kutoka shirika lishilo la kiserikali la World Vision Tanzania kwa ajili ya kunawia mikono pindi wananchi wanapo toka msalani ili kupunguza maabukizi.
Akikabidhi msaada huo wa vibuyu chirizi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni thelasini na nane vitakavyo hudumia kaya zaidi ya elfu nne mia sita, Mratibu mradi wa Sustain kutoka World Vision Tanzania, ESTER BONIFACE amesema shirika hilo limekuwa likitoa huduma kwa watoto ambao ndiyo waathiriwa wakubwa na ugonjwa huo.
Akipokea msaada huo na kuzindua rasmi matumizi kwa wananchi na wanafunzi wa halmashauri ya wilaya na Singida, Mkuu wa Wilaya ya Singida, SAIDI AMANZI amewataka wananchi kuhakikisha wanatumia vyoo, ili kuepuka maabukizi mapya ya kipindupindu.
0 comments:
Post a Comment