Kundi la wanawake wa kujitoa mhanga limetekeleza mashambulio
kadha ya mabomu katika mji wa Maiduguri, kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Idadi ya waliofariki bado haijabainika lakini jeshi la Nigeria
linasema watu 14, wakiwemo wanawake hao wa kujitoa mhanga, wamefariki na
wengine 39 kujeruhiwa.
Mashambulio hayo yalitekelezwa Alhamisi jioni na yalilenga
misikiti, watu walipokuwa wamekusanyika kwa sala ya jioni.
Aidha, walishambulia nyumba ya kiongozi mmoja wa kundi la
kujilinda la wakazi.
Mashambulio sawia na hayo wiki mbili zilizopita karibu na
eneo lililoshambuliwa yaliua zaidi ya watu 100.
Kundi la Kiislamu la Boko Haram limekuwa likidaiwa kuhusika
katika mashambulio hayo ya kujitoa mhanga.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari aliahidi kukabiliana na
wapiganaji hao, na jana alikuwa akiongoza taifa hilo kuadhimisha miaka 55 tangu
kujinyakulia uhuru.
0 comments:
Post a Comment