Mwanamume aliyeua watu 77 nchini Norway ametishia kususia
chakula hadi afe, akilalamika kwamba anateswa gerezani.
Vyombo vya habari vinasema Anders Behring Breivik anadai
kutengwa kutoka kwa wafungwa wengine tangu Septemba 2, na kwamba huwa
anaruhusiwa kutoka nje ya seli yake saa moja tu kwa siku.
Breivik aliua watu 77 kwamba 2011 alipolipua bomu katikati
mwa Oslo kabla ya kufyatulia risasi mamia ya vijana waliokuwa wamekusanyika
katika kisiwa cha Utoya nchini humo.
Alihukumiwa kifungo cha miaka 21 jela 2012.
Madai hayo yake kwamba anawekwa katika hali mbaya ameyatoa
kwenye barua aliyoandika na kuituma kwa vyumba vya habari Norway na Sweden.
Kwenye barua yake, Breivik, 36, anasema hali ngumu gerezani
imemlazimisha kuacha kozi yake ya sayansi ya siasa aliyokuwa akisoma katika
Chuo Kikuu cha Oslo.
"Kusoma na kufanya mawasiliano ni jambo lisilowezekana
chini ya mazingira kama haya,” alisema kwenye barua.
Breivik alisema hali ikisalia ilivyo, atasusia chakula hadi
afariki dunia, kwa mujibu wa vyombo vya habari Norway.
Mkurugenzi wa gereza la Skien anakozuiliwa Breivik, Ole
Kristoffer Borhaug, aliambia BBC kwa sasa hakuna mtu anayesusia chakula
gerezani humo.
Waziri wa Haki wa Norway Anders Anundsen alikataa
kuzungumzia madai hayo ya Breivik, kwa mujibu wa gazeti la Dagbladet.
0 comments:
Post a Comment