Watu tisa wameuawa na wengine saba kujeruhiwa baada ya
kutokea shambulio la risasi katika Chuo kimoja katika jimbo la Oregon, Polisi
wameeleza.
Mtu mwenye silaha alifyatua risasi chuo cha Umpqua Alhamisi
asubuhi na baadae kuuawa aipokuwa akijibizana kwa risasi na Polisi.
Kuna habari za kukanganya kuhusu madhara yaliyojitokeza
lakini Afisa Polisi wa eneo hilo amesema Watu 10 wameuawa akiwemo muuaji huyo.
Polisi hawajamtambua muuaji lakini afisa mmoja ambaye
hakutaka jina lake litajwe ameviambia vyombo vya habari nchini Marekani kuwa
jina lake ni Chris Harper Mercer.
Sababu za muuaji huyo kutekeleza shambulio hazijajulikana,
ingawa Polisi wanasema wanafanyia uchunguzi ripoti kuwa alitahadharisha dhamira
yake katika mtandao wa kijamii.
Saa kadhaa baada ya shambulio, ambalo watu saba walijeruhiwa
Rais wa Marekani, Barack Obama ametaka kuwe na sheria kali za udhibiti wa
silaha.
0 comments:
Post a Comment