Zaidi ya walimu 245,000 hawatapata mishahara yao mwezi
huu,kufuatia mgomo wa nyongeza ya mishahara unaondelea kwa wiki ya sita sasa
kulingana na gazeti la nation nchini humo.
Wengi wa wale watakaopata mishahara ni wafanyikazi wa shule
ambao hawakujumuika katika mgomo huo.
Siku ya Alhamisi mahakama ya rufaa iliwagiza walimu kurudi
shuleni mara moja huku ikiwa mamilioni ya watoto wa shule hawaezi kwenda shule
kutokana na mgomo huo.
Mahakama ya Kenya imeiagiza serikali kuongeza mishahara ya
walimu kwa hadi asilimia 50,lakini serikali inapinga hilo ikidai kwamba haina
fedha za kuwalipa.
0 comments:
Post a Comment