Mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa taifa wa chama cha
siasa cha National League for Democrasy-NLD- na mwenyekiti mwenza wa umoja wa
katiba ya wananchi-UKAWA- Daktari Emmanuel Makaidi umeagwa leo katika viwanja
vya Karimjee na kuzikwa katika makaburi ya Sinza jiji Dar es Salaam.
Katika ibada fupi ya kuuga mwili wa marehemu Daktari
Emmanuel Makaidi iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo mgombea urais
kwa tiketi ya Chadema.Bw. Edward Lowassa, wazii mkuu mstaafu Fredrick Sumaye na
makamu mwenyekiti wa CCM Bwana Philip Mangula, mchungaji wa kanisa TAG
makumbusho Bwaba Davd Mwakwenda amewataka wanasiasa kuhacha kuombeana mabaya na
kutakiana amani ili kuwa na taifa lenye baraka.
Msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi
ameiomba jamii kuhacha kuhusisha matukio ya vifo yanayoendele kujitokeza na
harakati za kisiasa na kuwataka wanasiasa kutambua swala la amani ni la msingi
hivyo taifa likiingia katika uchaguzi mkuu kwa amani litakuwa limemuenzi marehemu
Daktari Emmanuel Makaidi.
Akiongea kwa niaba ya umoja wa katiba ya wananchi
Bwana James Mbatia amesema umoja huo umepata pengo kubwa kutokana na kifo cha
mwenyekiti mwenza marehemu Dkt Makaidi kwa kuwa imekuwa ikituma taaluma yake ya
sayansi ya siasa katika mipango yao, huku mwenyekiti wa Chadema Bwana Freeman
Mbowe akivita vyombo kisheria na mamlaka za kiserikali kutotumia nguvu ili
kwezesha uchaguzi kuwa huru na amani kama njia ya kumuenzi marehemu Dkt
Emmanuel Makaidi.
0 comments:
Post a Comment