Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda amewataka wawekezaji wa ndani
katika sekta ya sukari kuhakikisha wanaimarisha viwanda vyao kwa
kuzalisha sukari kwa wingi kutokana na mahitaji ya bidhaa hiyo
kuhitajika kwa watanzania wengi.
Waziri
mkuu Pinda amesema hayo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akizindua
nembo mpya ya kiwanda cha sukari cha Kilombero ambayo kwa sasa itakuwa
na mwonekano mpya.
Amesema mahitaji ya sukari hapa nchini yameongezeka hivyo sasa wawekezaji wa ndani wana wajibu wa kuimarisha viwanda vyao kwa kuongeza uzalishaji zaidi kwa mujibu wa mahitaji katika soko la Tanzania.
Mh. Pinda amesema viwanda vya ndano vya sukari vinawajibu mkubwa wa kuhakikisha kwamba vinakidhi mahitaji ya watanzania kwa kuwa vinazalisha sukari iliyo bora na yenye viwango vinavyohitajika.

0 comments:
Post a Comment