Serikali ya Tanzania imetoa taarifa kwa shirika la afya duniani (WHO)
kuhusu kuongezeka kwa ugonjwa kipindupindu nchini huku aina mpya ya
kirusi kungundulika jijini Dar-es-Salaam tarehe 25 Agosti.
WHO
inasema, ripoti ya hivi karibuni inaonesha kipindupindu kimesambaa
katika mikoa 13 nchini Tanzania na sasa kimefika kisiwani Zanzibar.
Christian Lindenmeyer ni msemaji wa WHO amesema wagonjwa 4,324 wa
kipindupindu wameriptiwa ikiwemo vifo 67 ambapo ugonjwa huo umeingia
visiwani Zanzibar ambako wagonjwa 106 wameripotiwa.
WHO inasema, kipindupindu kimeathiri pia Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC) ambapo visa zaidi ya elfu tatu vimeripotiwa pamoja na vifo
91.
Wakati huohuo huo watu kumi na saba wamepoteza maisha na wengine
miasaba themanini na tano wamelazwa katika vituo vinne kutokana na
ugonjwa wa kipindupindu katika halmashauri ya wilaya ya Singida kwa
kipindi cha kuanzia Septemba hadi Oktoba mwaka huu.
Kaimu mganga wa halmashauri ya wilaya ya Singida Dkt. Paul Maiga
amesema hayo wakati walipokuwa wakipokea vibuyu chirizi elfu nne mia
sita kutoka shirika lisilo la kiserikali la World Vision Tanzania kwa
ajili ya kunawia mikono pindi wananchi wanapotoka chooni kwa lengo la
kupunguza maambukizi .
0 comments:
Post a Comment