Viongozi wakuu katika serikali ya Zambia wanahudhuria siku kuu ya kitaifa ya kufunga na kuliombea taifa hilo ilikunusuru thamani ya sarafu yake.
Maombi hayo yameitishwa kutokana na mfumuko wa bei ya vyakula na
bidhaa nyingine muhimu mbali kuporomoka kwa uchumi wa taifa hilo
linalotegemea kwa kiwango kikubwa mauzo yatokanayo na madini ya shaba.
Kwa mujibu wa kanuni zilizotolewa baa zote na vilabu vya burudani vimefungwa.
Na si hayo tu waandalizi wa siku hii maalum ya maombi pia
wamehakikisha kuwa hakuna uraibu wowote unaoendelea kwa leo hata mechi
za kandanda ambayo hupendwa sana nchini humo zimeaahirishwa.
Thamani
ya sarafu ya Zambia, Kwacha, imedorora mno na kupoteza takriban nusu ya
thamani yake katika kipindi cha miezi 9 iliyopita.
Kufikia sasa Sarafu hiyo imepoteza asilimia 45% ya thamani yake ikibadilishwa na dola ya Marekani.
Hali
hii watafiti wa maswala ya kiuchumi wanasema imetokana na mfumuko wa
bei ya shaba ambayo imeanguka mno kufuatia mfumuko katika uchumi wa
mteja wake mkuu China.
Rais Edgar Lungu anatarajiwa kuhutubia taifa hilo wakati wa hafla hiyo kubwa inayofanyika katika mji mkuu Lusaka.
0 comments:
Post a Comment