Image
Image

Jarida la Forbes latoa orodha ya matajiri 10 zaidi barani Afrika.


Jarida la Forbes hutoa kila mwaka orodha ya mataji wenye milki nyingi barani Afrika.
Matajari hao, wengi wao hujishuhulisha na biashara ya saruji, marembo, uuzaji wa vyakula.
Wengi wa matajiri hao hutokea nchini Afrika Kusini, Nigeria na Misri.
Miongoni mwa matajiri hao Afrika yumo mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 42.
1. Aliko Dangote, Nigeria.
Mwafrika tajiri zaidi ulimwenguni ana umri wa miaka 58 anamiliki bilioni 15,7 sarafu za Marekani.
Alianza biashara baada ya kuchukuwa mkopo wa pesa 2,300 sarafu za Ulaya kutoka kwa mjomba wake na kuanza biashara ya saruji alipokuwa na miaka 20.
2. Johann Rupert, Afrika Kusini.
Johann Rupert, raia huyo wa Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 65 anamiliki kiwango cha pesa bilioni 7,1 ambazo ni urithi kutoka baba yake Anton Rupert ambae alikuwa akifanya biashara ya tumbaku.
3. Nicky Oppenheimer, Afrika Kusini
Mrithi wa mali katika kampuni ya babu yake ya De Beers mwenye asili ya kiyahudi aliehamia Afrika Kusini.
Mali yake inakadiriwa kuwa bilio 6,7 sarafu za kimarekani.
4. Christoffel Wiese, Afrika Kusini
Kwa jina maarufu « Christo » ana umri wa miaka 74 anajihusisha na uuzaji wa nguo.
Mali yake ni bilioni 6,3 safaru za Marekani.
5. Nassef Sawiris, Misri
Nassef Sawiris ana umri wa miaka 54, mali yake ni bilioni 6,3 sarafu za Marekani.
Kampuni ya familia Orascom Construction inajihusisha na ujenzi na uuzaji wa saruji.
6. Mike Adenuga, Nigeria
Tajiri wa pili nchini Nigeria ana umri wa miaka 62 anajihusisha katika sekta ya mawasiliano.
Alifungua kampuni ya Global Communications (Globacom) mwaka 2006.
Mali yake ni bilioni 4 sarafu za Marekani.
7. Mohamed Mansour, Misri
Mansour ana umri wa miaka 67 na anaogoza mradi wa familia wa Metro unaojıhusisha biasha katiaka vituo vıkubwa vya biashara nchini Misri ikiwemo Palm Hills , kampuni ya uuzaji wa vifaa vya ndani.
Mali yake ni bilioni 4 sarafu za Marekani.
8. Nathan Kirsh, Swaziland
Kirsh ana umri wa miaka 83 na mwenye asili ya kiyahudi mali yake inakadiriwa kuwa bilioni 3,9.
Anajihusisha na uuzaji wa vifaa vya ndani katika kampuni ya Swazi Plaza Properties na uuzaji wa viungo.
9. Isabel Dos Santos, Angola
Mtoto wa kwanza wa rais José Eduardo Dos Santos, madarakani tangu mwaka 1979 tajiri mkubwa wa kike barani Afrika.
Mali yake ni bilioni 3,1 sarafu za Marekani.
Mke wa Sindika Dokolo raia wa DR Congo anaejihusisha na biashara ya vinyago.
10. Isaad Rebrab, Algeria
Muhasibu mwenye umri wa miaka 71 anamiliki bilioni 3,1 sarafu za Marekani.
Isaad anajihusisha na biasha ya mafuta ya kupikia, sukari na vinywaji.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment