Mgombea urais kupitia Chadema kwa umoja wa UKAWA
Edward Lowassa ameitakia kila la Kheri timu ya taifa ya soka Taifa Stars katika
mchezo wake dhidi ya Malawi wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za dunia mwaka
2018 kesho jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa anayokila sababu kuitakia mema Taifa
stars kwani kila uchao Tanzania kuonekana kichwa cha mwenda wazimu katika soka
anaamini haiwezekani kwani vijana hao wanauwezo mkubwa tu na watanzania wengi
wanapenda soka licha ya kuwa wanyonge kwa timu za Tanzania kushindwa kwa kuto
kufanya vyema katika michuano ya kimataifa lakini nivema kujitokeza
kuishangilia timu ya Taifa na kuibuka na ushindi ambao utakuwa ni ushindi wa
Taifa.
Amesema naomba msukumwe na joto na hamasa iliyopo
nchini hivi sasa ya MABADILIKO,kuleta mabadiliko uwanjani,kwa kuwafunga Malawi
na kutupa raha watanzania.Alisema Lowassa.
Timu ya Taifa stars chini ya kocha wao mzalendo
Charles Boniface Mkwasa ambaye anainoa Mh.Lowassa amempongeza na kumtakia kila
la Kheri katika kuleta ushindi nyumbani ambapo alisema kuwa.
Katika ilani yetu ya uchaguzi, michezo itapewa
kipaumbele makhsusi ili kuondokana na kuwa kichwa cha mwendawazimu.
Hata hivyo Mh.Lowassa ameongeza kwa kusema kuwa
Ushindi watakao upata Stars utamzizidishia hamasa ya kuliangalia soka na
michezo mingine kwa umakini zaidi,atakapopewa ridhaa ya kuingia madarakani.
Aidha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza
viingilio vya mchezo wa Jumatano kati ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Malawi
(The Flames) kuwa ni shilingi elfu kumi tu (10,000) katika mchezo huo wa
kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Viingilio vilivyotangazwa ni kiingilio cha juu
kabisa kwa mchezo huo shilingi elfu kumi (10,000) kwa viti vya VIP B & C,
huku viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani ikiwa ni shilingi elfu tano
(5,000).
Stars inayonolewa na kocha mzawa Charles Boniface
Mkwasa imeendelea kujifua katika viwanja vya Gymkhana na uwanja Taifa jioni
kujiandaa mchezo huo wa Jumatano dhidi ya Malawi, huku wachezaji wakiwa wenye
ari na morali ya hali ya juu kuelekea kwenye mechi hiyo.
Wachezaji 22 wapo kambini akiwemo mshambuliaji
Mrisho Ngasa anayecheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini aliyeripoti jana
mchana kambini, huku wachezaji wawili Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu
wakitarajiwa kujiunga na wenzao leo wakitokea Lubumbashi – Congo DR.
Wakati huo huo timu ya Taifa ya Malawi (The Flames)
imewasili nchini jana saa 4 asubuhi na kufikia katika hoteli ya De Mag iliyopo
Mwanayamala, ambapo kikosi hicho leo kimefanya mazoezi asubuhi katika uwanja wa
Boko Veterani.
Waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Somalia, kamisaa
na mtathimin waamuzi wa wanatarajiwa kuwasili leo nchini na kufikia katika
hoteli ya Protea iliyopo Oysterbay.
Mwamuzi wa kati ni Hagi Yabarow Wiish (Somalia),
akisaidiwa na Hamza Hagi Abdi (Somalia), Salah Omar Abubakar (Somalia), mwamuzi
wa akiba Bashir Olad Arab (Somalia), mtathimini wa waamuzi Sam Essam Islam
(Misri) na kamisaa wa mchezo ni Muzambi Gladmore (Zimbabwe).
0 comments:
Post a Comment