Mamlaka ya udhibiti wa chakula na
dawa nchini Tanzania TFDA kanda ya mashariki imefanikiwa kuharibu tani 3 za
bidhaa feki ikiwemo pamoja na maziwa ya watoto wenye thamani ya zaidi ya
mamilioni ya shilingi jijini Dar es Salaam.
Bidhaa hizo feki zimeteketezwa
kwenye Supar maket zaidi ya 126 ambapo wakaguzi wa TFDA wamesema jumla ya
maduka 40 kati 126 yamekutwa hayana vibali vya biashara na kuuza maziwa ya
watoto ambayo yapo chini ya kiwango ikiwa ni pamoja na kutokuwa na lebo.
Wakaguzi hao wametoa w wito kwa wafanya biashara
wote nchi nzima kuwa makini na baadhi ya bidhaa zote zinazoingizwa nchini
kinyume cha utaratibu unaokidhi viwango husika vya mamlaka pamoja na kuwa na
vibali yvote kabla ya kufungua biahara hiyo.
Mamlaka ya chakula na dawa TFDA imekuwa ikifanya
zoezi hilo la uteketezaji bidhaa zisizo kuwa na ubora sehemu mbali mbali nchini
ili kuwaepucha wanunuzi na watumiaji wa bidhaa hizo kukumwa na madhara
yatokanayo na bidhaa zisizo na ubora na kuzitekeza.
0 comments:
Post a Comment