Mgombea Urais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, ANNA MGHWIRA amesema iwapo atapewa ridhaa ya kuiongoza nchi, Serikali yake itatatua matatizo ya ardhi yanayoukabili Mkoa wa Arusha hasa katika Wilaya ya Arumeru kwa kurudisha umiliki wake kwa wananchi.
Akihutubia mikutano ya hadhara katika Kata za Makiba na Sing'sin katika Jimbo la Arumeru Mashariki Mkoani Arusha, amesema serikali yake itarudisha mashamba yote na kutoa pembejeo kwa wananchi ili watumie kuendeleza kilimo.
Akihutubia mkutano mwingine katika viwanja vya Ngarenaro Jijini Arusha, mgombea huyo wa Urais pekee mwanamke katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, amesema serikali yake haitakuwa ombaomba na itategemea zaidi mapato ya ndani kuendesha nchi.
0 comments:
Post a Comment