Bado siku kadhaa kuweza kukamilisha utaratibu mzima wa kupata kiongozi wa Taifa la Tanzania atakaye tuongoza baada ya kipindi cha Rais Jakaya Kiwete kufikia ukikongi baada ya kutumikia miongo kumi ya ya uongozi wake kwa mijibu wa katiba ya nchi.
Wakati siku zikiendelea kusogea bhasi siasa nayo inaonesha kushika kasi kweli kweli nchini Tanzania ambapo miongoni mwa wananchi haswa wakiwa wanashabikia vyama vyao vilivyo simamisha mgombea kila mmoja wao huonekana anashauku kubwa mgombea wa chama anacho shabikia kushika dola.
Amani na utulivu ndivyo vitu vinavyo sisitizwa kila uchao katika uchaguzi huu kwamba watu wasijeshabikia sana siasa wakajisahau na wakavunja sheria na hali ambayo itabidi mamlaka husika kuchukua mkondo wake jambo linalo tajwa lisije leta machafuko.
Kupitia ukurafa wa Facebook moja ya Mwanahabari na mchambuzi mzuri tu ameweza kuandika machache na haswa kuwakumbusha watanzania nijinsi gani baada ya uchaguzi maisha yataendelea hivyo nini wafanye na nini wasifanye....Endelea.
Na:Abel Musatta.
Tanzania kumekuwa na mambo
yanayozungumzwa kuhusu uchaguzi mkuu 2015 ama kiushabiki au kiushindani kuhusu
mabadiliko. Haikuishia kwa
wananchi wa kawaida pekee bali viongozi wa dini na dini zao, vyombo vya habari
kwa kuikiuka mizani ya uandishi hata vyombo vya habari vikubwa vyenye nembo ya
super brand vinatekwa na wimbi kubwa la wasomaji hivyo uandishi kuangalia soko
zaidi kuliko maslahi ya Taifa kwa kigezo ukiandika habari Inayohusu Mgombea
fulani au chama fulani utauza ama hautauza sana, kushuka kwa mauzo ni hatari
sana kwa kampuni lakini kuandika habari pasipo kuzingatia vigezo na mashariti
ya uandishi kunapelekea kufa kwa taifa. ukiwa ni mwanaharakati wa maendeleo ya
taifa letu inakupasa kulitangaza taifa zaidi ya chama kwani uongozi wa nchi ni
mfumo hautofautiani na ndoa. Ndoa hazifanani ila mfumo wa ndoa ni ule ule. MIMI
NATAKA MABADILIKO BORA SI BORA MABADILIKO sipotezi kura yangu kwa kujaribu
nisichokijua. Kubadili chama tawala si kubadilili mfumo bali maamuzi yangu
yanaweza kubadili mfumo hata kikiwa chama fulani, Mabadiliko ya kweli yanaanza
na mtu mmoja kujitambua na kuchukua hatua kwa kuweka vipaombele vyake hii
inamaana mimi sipendi kiongozi anaetumia muda wooote kuponda mtu ama chama
fulan bali yule tu anayeniambia taifa linatoka wapi na linakwenda wapi yeye
atafanya nini kutukwamua pale tulipo kwama.
0 comments:
Post a Comment