Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema
kazi bado ni ngumu pamoja na mwenendo mzuri wa kikosi chake.
Pluijm raia wa Uholanzi amesema
Ligi Kuu Bara ambayo wao ni mabingwa inaonekana itakuwa ngumu kwa muda wote.
“Ligi haiwezi kupungua ugumu, itakwenda hivi. Hata kama kuna timu zitajigawa kwa maana ya ubora lakini haziwezi kuwa chache.“Hata ukiwa na timu tano au sita katika ligi ambazo ni imara,maana yake ligi ni ngumu na inatakiwa kupambana mwanzo hadi mwisho,”alisema Pluijm.
Yanga imecheza mechi sita, imetoka sare moja na sasa
iko kileleni ikiwa na pointi 16, sawa na Azam FC.
Yanga na Azam FC ndiyo timu pekee ambazo
hazijapoteza hata mechi moja.
0 comments:
Post a Comment