Image
Image

Ndege ya JWTZ yaanguka baharini.

MARUBANI  wawili  wa kikosi cha jeshi la anga wamefariki baada ya ndege ya mafunzo ya  Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ) kupata hitilafu na kuanguka  eneo la Silversands Msasani katika kisiwa cha Mbudya,   Dar es Salaam.
Taarifa za kuanguka kwa ndege hiyo zilianza kusambaa kupitia mitandao ya jamii jana asubuhi   zikieleza kuwa  wavuvi walikuwa wa kwanza kutambua ajali hiyo baada ya   kuona kofia ngumu.
Akizungumza na Mtanzania Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano  wa JWTZ, Kanali Ngemela Lubinga  alisema tukio hilo lilitokea jana saa 3:30 asubuhi baada ya injini  ya ndege hiyo ya mafunzo kupata hitilafu na kuanguka katika kisiwa hicho.
“Baada ya hitilafu walijaribu kuruka na vifaa vya usalama walivyokuwa navyo kwenye ndege, lakini walipofika chini kulikuwa na maji walipojaribu kuogelea wakazama,”alisema Kanali Lubinga.
Kanali Lubinga aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Luteni Kanali Karikisio Ndongolo ambaye alikuwa mkufunzi na Kapteni Gaudenci Hamisi aliyekuwa  rubani, wote wa kikosi cha anga.
Alisema ndege hiyo ilikuwa haina jina wala namba kwa kuwa ilikuwa ya mafunzo.
Msemaji huyo wa jeshi alisema taratibu za kuitafuta miili hiyo zilikuwa zikiendelea mpaka jana ambako kikosi cha wana maji wakiwa na boti maalum   na vifaa vingine kilikuwa katika eneo hilo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment