Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec),imewataka wasimamizi wa uchaguzi
nchini na vyombo vya usalama kutoruhusu makundi ya watu kukaa karibu na
eneo la kupigia kura kwa kisingizio cha kulinda kura kwa kuwa
itasababisha uvunjifu wa amani.
Mwenyekiti wa Nec, Jaji mstaafu Damian Lubuva (Pichani), alitoa
agizo hilo jijini Dar es Salaam jana wakati wa mkutano wa pamoja na
waratibu wa uchaguzi wa mikoa,wasimamizi wa uchaguzi na makamanda wa
polisi wa mikoa na kanda maalum.
Alisema changamoto zinazojitokeza katika chaguzi zilizopita ni
pamoja na kuwapo kwa makundi ya vijana wanaohisiwa kuwa wafuasi wa vyama
vya siasa kuwatisha wapigakura hasa akinamama ili wasiende kupiga kura.
Jaji Libuva alisema mawakala wa vyama wataruhusiwa kuwapo katika vituo
vya kupigia kura na wajibu wao ni kuangalia sheria, kanuni na taratibu
zilizowekwa na Nec zinazingatiwa katika mchakato wa kupiga kura,
kuhesabu na kutangaza matokeo na pia kulinda maslahi ya chama na
wagombea.
“Ni muhimu uwepo ushirikiano mkubwa kati ya watendaji wote wa kazi
hii, serikali, vyombo vya ulinzi na usalama, vyama vya siasa na wadau
wengine wote. Nawasihi muwe na ushirikiano mzuri na kuwa karibu sana na
Nec wakati wote mtakapokuwa mnahitaji ufafanuzi au maelekezo katika kazi
zenu,” alisema.
0 comments:
Post a Comment