WATU zaidi ya wanane wanahofiwa kufa baada ya kufukiwa na kifusi cha
udongo katika machimbo ya Nyangarata katika Kata ya Lunguya Wilaya ya
Kahama mkoani Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha alisema tukio
hilo lilitokea juzi asubuhi baada ya watu wapatao 20 kuingia katika
shimo la uchimbaji dhahabu na kifusi hicho kikaanguka wakiwa ndani.
Alisema ingawa idadi kamili juu ya waliokuwa ndani ya
shimo inakadiriwa kuwa 20 lakini baada ya ufuatiliaji wa kina
inakadiriwa iwapo kuna watu watakuwa walibakia ndani ya shimo hilo
idadi yao inaweza kuwa wanane ingawa
wachimbaji hao wanadai wanaweza kuwa 11.
wachimbaji hao wanadai wanaweza kuwa 11.
Kamanda alisema jitihada za serikali kuhakiki na kufuatilia
watu ambao wanaweza kuwa wamefukiwa ndani ya shimu hilo
zinaendelea kufanyika kwa kuwa baadhi ya wanaotajwa kufukiwa simu
zao zimekuwa zikiita hali inayoonyesha kuwamo kwao shimoni.
Diwani aliyemaliza muda wake katika Kata ya Lunguya, Benedict Manwari
alisema mpaka sasa idadi ya watu waliookolewa baada ya kuangukiwa na
shimo hilo ni 11 ambao wamejeruhiwa sehemu na kukimbizwa kwenye Kituo
cha Afya cha Luguya kwa matibabu.
Alisema kwa sasa wanaendelea na jitihada za kuokoa wachimbaji wengine
ambao inasadikika bado wamo ndani ya mashimo kwa kushirikina na kikosi
cha uokoaji kutoka katika Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu.
Naye Ofisa Madini Mkazi wa Wilaya ya Kahama, Sophia Omary alisema
amelazimika kusafiri kwenda eneo la tukio kuangalia machimbo hayo na
jinsi uokoaji unavyofanyika.
0 comments:
Post a Comment