Madereva wa mabasi ya Daladala Mkoani Morogoro,wamesitisha kutoa huduma ya usafiri katika mji huo na kufanya mgomo.
Madereva hao wanapinga kukamatwa madereva wenzao wawili na kuzuiliwa kituo cha Polisi kwa zaidi ya siku sita bila ya kupelekwa mahakamani wala kupewa dhamana.
Wamewataka Polisi kutenda haki ikiwa ni pamoja na kuwaachia madereva hao.
Uongozi wa Mkoa wa Morogoro haujatoa kauli yo yote kuhusiana na tukio hilo na walikuwa wakikutana kupata ufumbuzi wa mgomo huo.
Kutokana na mgomo huo wakazi wa Mji wa Morogoro tangu alfajiri wamekosa usafiri wa Daladala na kulazimika kutembea kwa miguu, wanafunzi na wafanyakazi kuchelewa kufika kazini na shuleni na wafanyakazi wengine kulazimika kutafuta usafiri mwingine ikiwmo pikipiki.
0 comments:
Post a Comment