Katika kukabiliana na vitendo
vinavyotokea mara kwa mara
mkoani Kagera vya uchomaji moto
makanisa ya madhebebu ya kikristo ambavyo vinavyofanywa na watu wasiojulikana,baadhi ya viongozi wa madhehebu hayo mkoani
humo wameelezea msimamo wa
pamoja wenye lengo la kukomesha vitendo
hivyo ambavyo vimeanza kuonyesha viashiria vya uvunjifu wa hali ya amani.
Kwa nyakati tofauti viongozi wa hao
ambao ni pamoja Elisa Buberwa Askofu wa kanisa la kiinjili la kirutheri Tanzania
wa diosisi ya kaskazini Magharibu na Desderius Lwoma askofu wa kanisa katoriki
wa jimbo la bukoba, wamesema katika kukomesha vitendo vya uchomaji moto
makanisa kuwa watahakikisha wanawahamasisha waumini wa madhehebu ya kikristo
ili wachukue uamzi wa kuyalinda kwa nguvu zote makanisa yao wanayotumia
kumuabudu mwenyezi mungu.
Kwa upande wake, Haruna kichwabuta
ambaye ni Sheikh wa mkoa wa Kagera amelaani vitendo vya uchomaji moto makanisa ya madhehebu ya
kikristo, pamoja na kulaani vitendo hivyo amewaomba waumini wa madhehebu ya dini
kuthaminiana na kila mtu kuheshimu dhehebu la mwenzake ili waweze kuimarisha
mshikamano.
Nao baadhi ya viongozi wa vyama vya
siasa wamewatahadhalisha wananchi kwa kuwataka wasichanganye masuala ya siasa
na vitendo vya uchomaji
moto wa makanisa ya madhehebu ya kikristo, kwa nyakati tofauti wamesema wanaochoma makanisa moto ni
waharifu hivyo wanapaswa kushughulikiwa kama waharifu wengine.
Vitendo vya uchomai wa
makanisa katika mkoa wa
kagera vimekuwa vikiongezeka kila kunapokucha kwa mwenzi uliopita wa septemba
jumla ya makanisa saba ya madhehebu ya kikiristo yalichomwa moto, kufuatia
matukio hayo jeshi la polisi mkoani humo linawashikilia watu nane kwa tuhuma ya
uchomaji wa makanisa hayo na linaendelea kuwasaka watuhumiwa wengine.
0 comments:
Post a Comment