Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha ukombozi wa
umma (chauma) Mheshimiwa Hashimu Rungwe amesema hakunasababu ya serikali kuuwa
viwanda na watu kukosa ajira na kuahidi neema kwa wananchi wa mkoa wa Morogoro
endapo atapata ridhaa atahakikisha anafufua viwanda ili kurudisha ajira
za wananchi wa mkoa wa Morogoro.
Mheshimiwa Rungwe amepokelewa na umati wa wakazi wa
mji wa Morogoro ambapo akihotubia katika viwanja vya soko kuu la manispaa hiyo
amesema endapo atapata ridhaa ya wananchi kuwa rais wa jamuhuri ya muungano wa
Tanzania ataunda serikali ya mseto na kuahidi kutatua kero sugu za wananchi
zikiwemo elimu, matibabu bure kwa wanawake wajawazito, watoto chini ya umri wa
miaka mitano pamoja na wazee.
Akihotubia katika kituo cha mabasi cha Msamvu mjini
Morogoro Rungwe amesema wakati wa chama cha mapinduzi kuwatumia wananchi
kama daraja la kuwavusha kuchukua madaraka na badae kuwaacha wakiteseka na hali
ngumu ya maisha sasa umefika mwisho ambapo amewataka wananchi wakichague Chauma
ili kiwaletee maendeleo ya uhakika na endelevu.
Kwa upande wake mgombea mwenza wa chama hicho Issa
Abasi amewataka wananchi wa mkoa wa Morogoro kuacha kukichagua chama cha
mapinduzi kwa mazoea kwani hakina hati miliki ya kuendelea kuwa madarakani
kufuatia kushindwa kutatua kero za wananchi kwa zaidi ya miongo mitano sasa.
0 comments:
Post a Comment