Licha ya mwigizaji Zuwena
Mohamed(Shilole) kupewa adhabu na Baraza la sanaa nchini (BASATA) kutojishughulisha
na kazi zozote za sanaakutokana na kutumbuiza akiwa amevaa nguo za nusu uchi
nchini Ubelgiji msani huyo ametajwa kuwa sikio la kufa baada ya kuendelea
kutupia Picha zinazoonesha maungo ya mwili wake kwenye mtandao wake.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter shilole aliweka picha ikimuonesha akiwa kalala kwenye fukwe mwa moja ya Hoteli huku akiwa amevaa taulo na kuonesha mapaja yake na kutupia maneno yasemayo,Sina habari nipo zangu beach Napata upepo wa habari.Kutokana na maneno hayo baadhi ya watu walioiona picha hiyo walimtaka shilole kubadili tabia yake kwani yeye ni kioo cha jamiina amekuwa akifuatiliwa na watu wenye rika tofauti wakiwamo watoto.
Shilole usione sifa kwa hayo unayo yafanya jua kwamba wewe ni kioo cha jamii hivyo unatakiwa ujiheshimu ili watu waweze kuheshimu kazi yako .Alisema Nelson Jonathan mmoja wa watu waliopitia ukurasa huo wa shilole.
0 comments:
Post a Comment