Mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku amebaini kwamba
angependa kucheza chini ya ukufunzi wa kocha wa Arsenal Arsene Wenger.
Lakini kabla ya hatua hiyo angependa kupewa fursa ili
kumthibitishia kocha Jose Mourinho, meneja ambaye alimuuza kwa madai kwamba
alikuwa mchezaji wa ziada katika kikosi cha Chelsea.
Mshambuliaji huyo alikuwa akijibu maswali kuhusu ni kocha
gani angependa kumchezea.
Akizungumza na gazeti la Le Vif nchini Ubelgiji, Romelu
Lukaku:''Mourinho ni wa kwanza,{Pep} Guardiola halafu Wenger''.
Lukaku hakupata fursa ya kung'ara katika kilabu ya Chelsea
ambapo alihudumia mda wake wa miaka mitatu kwa mkopo katika vilabu vya Wst Brom
kabla ya kuelekea Everton kwa uhamisho wa kudumu.
0 comments:
Post a Comment