Image
Image

Watu wenye ulemavu wamtaka Rais ajaye kushirikiana nao kukomesha ubaguzi na Mauaji.

                    Moja kijana Mlemavu akizungumza(Picha na Maktaba).
Muungano wa Vyama vya Walemavu Wasioona na Albino nchini wamemtaka Rais ajaye  na Serikali yake kushirikiana na walemavu kwenye ngazi za uamuzi  katika harakati za kutokomeza matukio ya ubaguzi, unyanyasaji na mauaji watu wa jamii hiyo.
Wakizungumza kwenye kongamano la kujadili matatizo yanayowakabili  wasioona shuleni katika Mkoa wa Dodoma  wamesema matukio ya ukatili yanayoikabili jamii hiyo yanashindwa kudhibitiwa ipasavyo kutokana na asilimia kubwa ya watu wenye dhamana ya kuzuia matukio hayo wakiwemo viongozi kutoguswa moja kwa moja na ukatili huo kutokana na wao kutokuwa jamii hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Wanawake na Watoto wa Chama cha Wasioona Tanzania, REHEMA DARUWESHI amesema bado jamii ya walemavu wasioona na jamii ya Albino shuleni inakabiliwa na matatizo mbalimbali katika masomo yao yanayotokana  na kutokuwepo kwa ushirikiano kwenye mamlaka husika pamoja na ukosefu wa fedha.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment