Kumekuwepo juhudi za asasi za kiraia na vyombo vya habari kuandaa midahalo ya wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Juhudi hizi zimefanywa kwa nyakati na namna tofauti ili kukidhi kiu ya Watanzania kuwapima wagombea hao kwa kuwauliza maswali muhimu kabla ya kuwapa ridhaa ya kuwaongoza.
Kwa sasa mashirika ya CEO Roundtable Tanzania, Tanzania Media Foundation (TMF), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), na Twaweza wameungana katika kuendeleza juhudi za kufanikisha mdahalo huu mahsusi.
Mdahalo huu utatoa fursa ya kipekee kwa wananchi kuuliza maswali muhimu kwa wale wanaoomba ridhaa yao ya kuwawakilisha na kuwaongoza. Mdahalo huu pia unawapa fursa wagombea Urais kuweka wazi ajenda zao kwa nchi yetu ili wananchi wazipime. Hivyo, tunatoa fursa kwa wananchi kuwasilisha maswali yao kwa wagombea Urais kuanzia leo hadi Ijumaa Oktoba 16. Maswali yanaweza kuwasilishwa kwa barua pepe, ujumbe mfupi wa maneno (SMS), mitandao ya kijamii au kupelekwa moja kwa moja kwenye ofisi ya asasi yoyote iliyotajwa hapo mwanzo.
Tumevialika vyama vya siasa vyenye wagombea Urais Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na wagombea ubunge wa majimbo yasiyopungua 55, kushirikisha wagombea wao wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tumevialika vyama husika kuchukua fursa hii ya kipekee na ya kihistoria kuwaonesha watanzania kuwa wako tayari kujibu moja kwa moja, maswali ya wapiga kura, na kuonesha kuwa serikali watakayounda baada ya uchaguzi itasimama bega kwa bega na wananchi.
Mpaka sasa, vyama vifuatavyo vimethibitisha ushiriki wao: Alliance for Democratic Change (ADC), Alliance for Change and Transparency - Wazalendo (ACT-Wazalendo) na Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA).
Mdahalo wa wagombea Urais umepangwa kufanyika Jumapili tarehe 18 Oktoba 2015. Tunaendelea kuwashawishi wagombea wa vyama vilivyobaki ili wathibitishe ushiriki wao kwenye tukio hili la kihistoria. Tumetuma barua rasmi kwa vyama vyote na tunawafuatilia ili wathibitishe ushiriki wao mapema iwezekanavyo.
Tutakutana na wawakilishi wa vyama vitakavyoshiriki Alhamisi tarehe 15 Oktoba 2015, ili kukubaliana sheria na kanuni za mdahalo. Tutakuwa na mkutano na wanahabari kutangaza sheria na kanuni hizo kwa wananchi siku ya Ijumaa tarehe 16 Oktoba, 2015.

0 comments:
Post a Comment